Kamdomo tu kiuno kimepoa poooh 😂 kiuno cha baridi kama damu ya nyoka muasi 🤸....mie huyu nijutie kukuacha wewe thubutu 😂😂😂😂😂" Ariana alikurupuka ndotoni akiwa ana pumua kwa kasi kama kakimbizwa na Simba mwenye njaa kali. Ni mwepesi wa kulia huyu acha aanze kulia huku akimtukana ex wake 😭.
Kilio chake kilikuwa kikubwa kiasi cha kumuamsha Mfanyakazi wake wa ndani.
"Ariana usiniambe bado una kumbuka kichambo cha Mike....unatakiwa upate Mwanaume atakaye kupamba kwa maneno matamu unatakiwa upate Mwanaume asiyejali kuhusu kiuno wala ukubwa wa nyonyo 😭 hili ni balaa sasa yaani kila ukilala tu anakuijia ndotoni. I don't know nifanye nini uwe sawa" Eva aliongea huku akilia.
"Eva unanisaidia kulia?....unanihurumia huna haja ya kunihurumia niliyataka mwenyewe. Nilimuamini huyo mtu nikijua ana akili timamu lakini ghafla tu aliniwakia kwa maneno magumu hasa baada ya kutembea na Mimi mara moja tu " Ariana alijihurumia na kujicheka pia
"Tafadhali sana naomba usihuzunike "
"Wacha niende club ni kajipoze "
"Ukienda club ndio una haribu kabisa mambo, tafadhali hebu njoo tupige magoti hapa chini nikuombee, hii hali ya kukumbuka maneno makavu ya yule mjinga hayatajirudia tena " Eva alitoa pendekezo, si unajua tena ni mlokole aliyeshika dini.
"Tunasali nikiwa nimevaa hivi hivi " Ariana aliuliza huku akichora plan kwa kichwa yake ni muoga sana wa kufanya maombi. Si unajua tena tabia ya Eva akikaa gotini ni mpaka kupambazuke.
"Hapana, jifunike shuka tu huna haja ya kuwaza gauni " Eva aliongea huku akipiga magoti
Ariana alichukua shuka kisha akashuka magotini, ile Eva anaanza kusali tu....Ariana alitoroka ....alizunguka nyuma ya nyumba akachukua vinguo vyake vya kihuni vilivyokuwa kwenye kamba.
Hakutaka kuchukua gari wala pikipiki alichukua zake kibaiskeli akiogopa kumkwaza Eva kwa ngurumo .
Ilikuwa ni saa saba usiku lakini hakuogopa kunyonga kibaiskeli chake.
Si unajua tena maeneo ya Mijini watu hutafuta pesa hadi majogoo basi alipaki kibaiskeli chake akasogea kwenye duka lililokuwa wazi akanunua maji ya kunywa.
Ile anarudi hivi, alishangaa kuona baiskeli yake inaondoka
"Mmmh kwani hili Jiji siku hizi lina vibaka " Ariana aliongea pekee yake asijue anaanzia wapi kupiga hata yowe, si unajua tena ni wa kishua alikubali baiskeli iondoke.
"Maombi ya Eva yameondoka na baiskeli yangu kama ningekaa magotini hadi kupambazuke kibaiskeli changu kisingeibiwa " Eva alijicheka kisha akaondoka zake, alihitaji kuingia club acheze mziki mpaka majogoo.
Alifanikiwa kupata Club moja kubwa inayojulikana kama Wakawaka.
Humu ndani watu hawalali, basi alijiachia kiuno chake kila aliyemshika hakumgombeza.
"Hiki kiuno si ndio ungekuwa unakionesha kitandani jii Mwanamke wewe kisa ni wa Kishua basi uno ndio lipoe namna hiyo. Ila kamdomo sasa " Ariana akiwa anakula zake bata sauti hii ilizunguka kichwani mwake.
Wacha apagawe na aone mziki kama unampigia kelele alitoka mbio akiwa hadi nje.
Alitafuta eneo zuri akajiegesha huku akijipepea.
"Kiuno kimepoa ....kwahiyo kwa siku zote hizo tumedate hakuona hata jema moja kutoka kwangu hakika ni ajabu sana" Ariana alijicheka.
Ghafla kibaiskeli kilisimama karibu yake, alinyanyua macho yake.
Tobaaa weeee alikutana na Mwanaume mzuri hajapata kuona tangu azaliwe, wacha apige kelele akihisi ni jini 😂😂😂 si kuna muda aliwahi kujinadi ni heri hata aolewe na jini sasa ndio alihisi jini limemfikia.
"Huyu vipi...." Yasin alijiuliza kisha akaipaki vizuri baiskeli, alinyoosha mkono wake akamziba mdomo Ariana, hakuwa hata na nia mbaya alihitaji wasikilizane tu na ndio maana alifanya hivi.
Vile sasa ananukia marashi si unajua tena ni mtoto wa Kiarabu.
Ariana hakuweza kustahimili alipoteza fahamu.
"Kosa langu ni lipi " Yasin alijiuliza, alitaka kumtelekeza lakini nafsi yake ilimkumbusha kutenda wema.
Alimpigia simu Daktari wake, dakika kumi hazikupita alifika.
"Huyu mtu kazimia, kama nitamuacha hapa basi wahuni watamfanyia ubaya. Hebu kaa naye mpaka pale atakaporejesha fahamu zake hii ni baiskeli yake. Akiuliza chochote kuhusu Mimi naomba uvunge haulewi kitu" Yasin alitoa maelekezo kisha akaondoka.
"Hivi ni kitu gani alikuwa anasema na Mimi " Daktari Mawenge alijiuliza kabla hajafikia muafaka Ariana alirejesha fahamu.
Hakutaka kujua nani yupo mbele yake alichomoka mbio kama hana akili nzuri 😂😂😂.
Pua zake zilikuwa zinanusa bado marashi ya Yasin acha akazane kukimbia huku akikemea.....ghafla tu aliparamiana na Eva . aliyekuwa kachoka kupita kiasi..... alionekana amemtafuta sana Ariana bila mafanikio.
"Eva weeee naomba uniombe 😭😭😭....nimekutana na jini mie"
"Na hata naweza kunusa marashi makali sana kwani alikukumbatia🙄" Eva mtu wa imani alizidi kumtisha Ariana.
0 Comments